June 22, 2026
ZANAB IMEPANGA KUFANYA UHAMASISHAJI JUU YA MASUALA YA ELIMU AFYA NA UCHUMI KWA WATU WASIOONA NA WENYE UALBINO
Timu ya ZANAB na Wizara ya Elimu kitengo cha elimu mjumuisho na stadi za maisha zafanya tathmini juu ya mahitaji ya kujifunza na ufikiaji kwa skuli kumi ikiwa tano katika wilaya ya Magharibi B na tano katika Wilaya ya Chakechake Pemba. Tarehe 12-13/05/2026 skuli zilizofikiwa kwa tathmini ni Fuoni kibondeni, Fuoni B msingi, Bwefum msingi,Kijitoupele A msingi na Dkt Samia amabapo tarehe 21-22/05/2026 kwa skuli za pemba zilizofikiwa ni pujini mjumuisho,madungu msingi,chanjaani msingi,michakaeni A msingi na Fiedelkasro sekondari.
Lengo kupata picha kamili ya hali ya mazingira ya skuli,vifaa na changamoto za kujifunzia kwa Wanafunzi wenye ulemavu na changamoto zinazowakabili walimu katika ufundishaji ili kupata suluhisho lake.